Kongamano la Ladies in Islam limethibitisha umuhimu wake katika kuwezesha wanawake wa Kiislamu katika nyanja mbalimbali za kibiashara, kifedha, uongozi, na ujasiriamali. Xerin Logistics Limited, ilikuwa miongoni mwa wadhamini walioshiriki katika kongamano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, posta jijini Dar es Salaam.Kwa kuhudhuria kongamano hili, Xerin Logistics ilipata fursa adhimu ya kujitangaza na kuanzisha uhusiano na wafanyabiashara wengine. Kupitia meza ya maonesho ya biashara, Xerin ilipata nafasi ya kushiriki katika mitandao ya biashara na hata kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Viwanda na Biashara. Kupitia ushiriki huu, Xerin Logistics imeonyesha dhamira ya kusaidia jamii kwa vitendo.
Zaidi ya kuwezesha wanawake kiuchumi, kudhamini kongamano hilo kuliwezesha Xerin Logistics kuchangia katika juhudi za kusaidia jamii. Fedha zilizopatikana katika kongamano hilo zitatumika kusaidia watu wenye mahitaji mbalimbali.
Hii inaonyesha jukumu la kampuni hiyo katika kukuza jamii na kuwezesha maendeleo endelevu. Kwa hakika, ushiriki wa Xerin Logistics katika kongamano la Ladies in Islam 2024 ilikuwa ni hatua muhimu katika kukuza uchumi na ustawi wa jamii kwa ujumla.